Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi huenda ataukosa mchezo dhidi ya Gwambina Fc baadae kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Aidha nahodha msaidizi Juma Abdul nae yuko kwenye hatihati ya kucheza leo baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union

Nafasi ya Abdul inaweza kuwa mtihani kwa kocha Luc Eymael kama atakosekana kwani hakuwahi kufanya mabadiliko kwenye nafasi hiyo tangu alipotua Yanga mwezi uliopita
Hata hivyo Paulo Godfrey 'Boxer' yuko fit, pengine leo atakuwa na nafasi ya kurejea kikosi cha kwanza
ADVERTISE HERE