Nimeleta password ya ushindi Yanga - Muro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Feb 2020
Nimeleta password ya ushindi Yanga - Muro

Msemaji na Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga Jery Muro amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kushuhudia burudani kutoka kwa mabingwa hao wa kihistoria katika mchezo dhidi ya Gwambina

Muro ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, yuko likizo na ameamua kuitumia likizo yake kuungana na viongozi kurejesha amsha-amsha

Akiwa sambamba na viongozi waandamizi wa Yanga katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Muro amesema amerejea na password ya ushindi Yanga

"Nawaambia mashabiki kesho njooni kwa wingi uwanjani kuna suprise yenu," amesema

"Kesho tunafungua ukurasa mpya kwa klabu yetu. Tumezungumza na kocha, wachezaji na tumewaambia kesho afe beki afe kipa, tunataka ushindi"

"Ile kampa kampa tena tunaitaka kesho, tunataka ushindi wa kuanzia goli nane"

"Viongozi wametimiza wajibu wao, wachezaji watimize wajibu wao na sisi mashabiki tutatimiza wajibu wetu"

"Kuanzia leo tunasema kulia basi, hatutakubali kuonewa wala kuhujumiwa na mtu yeyote. Leo tutalinda uwanja, wale waliozoea kutuhujumu waje waone. Hatutajali uwe mwenzetu, au yeyote, tutakushughulikia"

Muro amewataka wadau wote waliokuwa viongozi wa timu hiyo kipindi cha nyuma, wajitokeze kuunganisha nguvu

"Wale wote tuliokuwa sote wakati ule njooni tuunganishe nguvu. Viongozi wamefungua milango, tusibaki kulalamika tu kuwa timu inapotea. Wale mliokuwa mnamwaga upupu njooni mmwage, mliokuwa mkitoa magari, fedha njooni tufanye kazi tuirejeshe heshima ya klabu yetu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’