Tambwe, Kamusoko na Ngoma hatarini kuikosa Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Oct 2017
Tambwe, Kamusoko na Ngoma hatarini kuikosa Simba
Ikiwa imebakia siku moja kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Kocha wa Yanga, George Lwandamina, amesema kwake ni pigo kuwakosa nyota wake wa kimataifa, Amis Tambwe, Donald Ngoma na Thaban Kamusoko kwenye mchezo huo wa kesho.

Yanga ambayo inarejea leo jijini Dar es Salaam ikitokea Morogoro ilipoweka kambi kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Simba, itakosa huduma ya wachezaji hao ambao walibaki Dar es salaam kujiuguza majeraha yao.

Lwandamina amesema kuwa kukosa huduma ya nyota hao kwenye mchezo mkubwa na wenye upinzani kama wa kesho ni changamoto kwake.

“Nashukuru wachezaji wangu wapo katika ari nzuri, lakini kama mnavyojua Tambwe, Ngoma na Kamusoko hatupo nao huku (Morogoro) wapo Dar es Salaam wakiendelea kujiuguza, nilitamani sana kuwa nao kwenye mchezo wa Jumamosi kwa sababu ni wachezaji wenye uzoefu,” alisema Lwandamina.<

Alisema kuwa pamoja na kuwakosa nyota hao, hiyo haiwezi kuwa sababu ya kupoteza mchezo huo na wamejipanga kupambana ili kupata pointi tatu.

“Naamini wachezaji ambao ninao wanaweza wakaifanya kazi nzuri Jumamosi..., tunaye Ajibu (Ibrahimu) na Chirwa (Obbrey) kwenye safu ya ushambuliaji ambao wamekuwa wakifanya vizuri,” alisema Lwandamina.

Aidha, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, amesema kikosi cha timu hiyo kinarejea Dar es Salaam leo mara baada ya mazoezi ya asubuhi tayari kuwakabili vinara hao wa ligi kuu.

“Hatuna majeruhi miongoni mwa wachezaji tulionao huku (Morogoro) na tunaomba wachezaji wandelee kuwa katika ari nzuri, tunarejea kesho (leo)asubuhi tutaingia kambini mpaka siku ya mchezo,” alisema Saleh.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa hasa kutokana na ubora wa vikosi vya timu hiyo waliouonyesha kwenye michezo miwili iliyopita
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →