Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) na Muungano wa Wanasoka Duniani (Fifpro) wamebuni hazina ya kifedha ya Fifa FFP itakayokuwa ikishughulikia maslahi ya wachezaji ambao watakuwa na matatizo ya kulipwa au ambao dalili zote zinaashiria kwamba hawatawahi kulipwa na klabu zao
FIFA imetenga kiasi cha $4M ambazo zitawekwa katika hazina ya Fifa FFP hadi mwishoni mwa mwaka 2022 ambapo mgao wa fedha hizi utashuhudiwa
Wastani wa $3M zitatumiwa mnamo 2020, $4M mnamo 2021 na $4M mnamo 2022.
Aidha, $5M zitakazosalia katika hazina hiyo zitatumiwa kushughulikia malimbikizi ya mishahara ambayo wachezaji wa vikosi mbalimbali hawajalipwa kati ya Julai 2015 na Juni 2020.
"Kubuniwa kwa hazina hii kumechochewa na haja ya kushughulikia maslahi ya wanasoka ambao hawawezi kwa sasa kujikimu kimaisha kutokana na changamoto mbalimbali za kifedha zinazokabili waajiri wao duniani," alisema Rais wa FIFA, Gianni Infantino.
Maamuzi ya kubuniwa kwa hazina ya Fifa FFP itakayoanza kutekelezwa mnamo Julai 1, 2020 ni nafuu kubwa kwa wengi wa wachezaji na maafisa wa benchi za kiufundi ambao wanasubiri kulipwa mishahara yao na klabu mbalimbali duniani