Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara aliweka ujumbe ambao umeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kabla hajaufuta muda mfupi baadae
Katika ujumbe huo Manara ameonekana kuunga mkono madudu yanayofanywa na waamuzi kwa kuipendelea klabu ya Simba kuwa ni haki yao kwa kuwa wakati wa uongozi wa Jamal Malinzi Yanga nayo ilikuwa ikipendelewa
Aidha Manara amesema Simba itatwaa ubingwa kwa miaka kumi mfululizo yaani kuanzia 2020 mpaka 2030

Katika uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na mlinda lango Ramadhani Kabwili, pengine vyombo husika vinaweza kuanza na bosi huyo wa kitengo cha habari cha klabu ya Simba
ADVERTISE HERE