Eymael afunguka maendeleo ya kikosi chake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2020
Eymael afunguka maendeleo ya kikosi chake

Baada ya kushinda mechi nne mfululizo, kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema ameridhishwa na mwenendo wa kikosi chake kwani ameanza kuona mabadiliko ya uchezaji aliokuwa akiyahitaji

Hata hivyo amesema timu bado haijafikia katika kiwango anachokitaka

Mbelgiji huyo mwenye historia ya kushinda mataji kwenye kila ligi aliyofanya kazi, amesema lengo lake ni kuwa na kikosi imara kinachoweza kushindania ubingwa msimu huu hata hivyo amesisitiza ni lazima TFF ihakikishe ushindani unakuwa sawa kwa timu zote

"Timu imeanza kuwa na mwelekeo, itabadilika na kufika mahali ninapopataka, ni vigumu wachezaji kubadilika kwa wiki mbili au tatu, lakini tayari kuna mabadiliko yanaonekana kwenye kikosi na wachezaji mmoja mmoja, nafikiri tutafikia malengo, nafasi yetu si mbaya,"alisema

"Nimegundua ushindani uko katika baadhi ya mechi, ni wazi mechi hizo ni chache, lakini ili uwe na timu ya taifa bora, ni lazima uwe na ligi yenye ushindani na imara, nimetazama ligi ya hapa kuna matatizo ambayo yanapaswa yafanyiwe kazi, kuanzia waamuzi na wachezaji, kuna vitu vinahitaji kufanyiwa mabadiliko"

Kesho Jumamosi, Eymael ataiongoza Yanga kwenye mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting

Ni mchezo wa kisasi kwa Yanga ambayo ilipoteza mchezo wa duru ya kwanza ambao ulikuwa wa ufunguzi wa msimu kwa kufungwa bao 1-0 na maafande hao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’