Mshambuliaji wa Yanga Tariq Seif Kiakala hajawatumikia mabingwa hao wa kihistoria tangu kuanza kwa mwaka 2020
Kiakala aliyetua usajili wa dirisha dogo, aliifungia Yanga bao pekee kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United
Mchezo huo uliopigwa Disemba 30 mwaka jana, ulikuwa wa kwanza kwake, lakini pia ndio mchezo pekee aliocheza tangu asajiliwe
Kiakala alipata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa zaidi ya wiki nne
Alirejea kikosini na kuanza mazoezi mwishoni mwa mwezi uliopita
Pengine atahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi ili awe 'fit' kabla ya kuanza kuonekana kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael
Tariq ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga kutokana na umahiri wake katika kutumia nafasi kufunga mabao
Mwamba huyu ana tabia za ki-Amissi Tambwe na kwa Yanga hii inayotengeneza nafasi nyingi, anaweza kufunga mabao mengi Eymael atakapoanza kumpa nafasi