Mbinu za Eymael zinaibeba Yanga - Tshishimbi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Feb 2020
Mbinu za Eymael zinaibeba Yanga - Tshishimbi

Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema aina ya soka wanalocheza kwa sasa chini ya kocha wao mpya Luc Eymael linatoa nafasi ya kushambulia zaidi tofauti na awali.

Tshishimbi ameiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, alisema wakati wakiwa chini ya Mwinyi Zahera walikuwa wakicheza kwa kujilinda zaidi hasa katika michezo mikubwa huku wakitumia mipira mirefu kushambulia.

β€œKila kocha amekuwa na mbinu za namna yake. Zahera alikuwa bora kwa wakati wake, Eymael anapenda tucheze soka la kushambulia zaidi huku tukicheza pasi fupi fupi na kupiga ndefu penye ulazima wa kufanya hivyo,” alisema Tshishimbi.

Hata hivyo aina ya soka la Eymael, Tshishimbi alisema halijawachukua muda kulizoea pamoja na kuwa asilimia kubwa ya wachezaji ilikuwa imezoea soka la pasi ndefu.

β€œTulipata shida kidogo katika michezo miwili ya mwanzo ambayo tulicheza vizuri, lakini tukapoteza, baada ya hapo aina ya soka letu likawa linaendana na matokeo,” alisema.

Wakati akijiunga na Yanga, Eymael aliweka wazi aina yake ya soka huku akitoa ahadi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa watarajie soka safi na ushindi katika michezo mbalimbali.

Katika michezo mitano ambayo ameiongoza Yanga katika mashindano yote tangu akabidhiwe mikoba ya Zahera, Eymael ambaye ni raia wa Ubelgiji, ameifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi katika michezo mitatu na kupoteza miwili.

Yanga ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 31, kesho Jumatano watakuwa na kibarua kingine cha kucheza dhidi ya Lipuli FC.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’