Tujitokeze kwa wingi uwanja wa Uhuru Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2017
Tujitokeze kwa wingi uwanja wa Uhuru Jumamosi
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa amewataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanawahi kukata tiketi mapema na kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba, Jumamosi Oktoba 28.

AKizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga mtaa wa Jangwani, Mkwassa amesema uwanja wa Uhuru unachukua mashabiki wachache hivyo ni muhimu WanaYanga kununua tiketi kwa wingi ili kuweza kuipa sapoti timu yao katika mchezo huo ambao Yanga itakuwa mwenyeji.

Aidha, Mkwassa amewataka mashabiki kutofanya vurugu dhidi ya wapinzani wao akibainisha changamoto ya usalama kutokana na ukaribu wa majukwaa.

"Kwa ujumla maandalizi yapo vyema na hofu Yangu ni Usalama Wa uwanja kwakuwa ni mdogo,nivyema wanayanga tukawahi kuingia ukizingatia sisi ndiyo wenyeji", amesema.

"Tulijaribu kuomba Taifa lakini imeshindikana na bado hata hawajakabidhi Uwanja kwa serikali. Naamini miaka michache ijayo tutacheza na Simba hapahapa Kaunda"

Naye Afisa wa Habari wa Yanga Dismas Ten amewashukuru wanachama na mashabiki kwa kuendelea kukusanya michango ya kukarabati Uwanja Wa Kaunda.

Akizungumzia kuhusu hali ya kikosi Ten amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri ikiwemo wale ambao walikuwa majeruhi.

Benchi la ufundi litaamua kama liwajumuishe kwenye kikosi kitakachoivaa Simba Jumamosi au laa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’