Kitendo cha Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM kumleta nchini mtaalam wa soka la kisasa Carraca Antonio Domingoz Pinto, ni ishara ya dhamira ya kuifanya YangaΒ kuwa taasisi imara
Ni wazi GSM wanajiandaa kuwekeza 'mazima' Yanga, na hakuna shaka, ujio wa Pinto ambaye aliiongoza klabu ya Benfica kwa miaka 10, ni dalili njema
Kila Mwanayanga alikuwa akisubiri kuona hatua kama hizi zinachukuliwa ili kuirejesha timu katika makali yake
Kwa nini Pinto?
Ukingumzia soka la Ureno, lazima utaje klabu ya Benfica kwani ndio timu yenye mafanikio zaidi kuliko timu yoyote nchini humo
Kama ilivyo kwa Yanga, Benfica ndio timu yenye mashabiki wengi zaidi ndani na nje ya Ureno kuliko wapinzani wao Fc Porto na Sporting
Huko Ureno timu hii inafahamika kama timu ya Wananchi!
Benfica ina wanachama zaidi ya 230,000 na mashabiki zaidi ya Milioni 14 kutoka ndani na nje ya Ureno
Barani Ulaya klabu hii inatajwa kuwa timu yenye uungwaji mkono zadi kwenye Taifa lake (Ureno) kuliko timu yoyote
Asilimia 47 ya Wananchi wa Ureno wanaiunga mkono Benfica
Pinto amekuwa sehemu ya mafanikio ya timu hii katika kipindi cha miaka 10 akiwa Mtendaji Mkuu
Mwaka 2000 uongozi wa timu hiyo chini ya Rais Joao Vale e Azevedo waliunda kampuni ambayo ilipewa jukumu la kuisimamia Benfica Fc
Leo hii klabu hiyo inamiliki vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo kituo kikubwa cha televisheni
Wana Academy nzuri za kulelea vipaji ikiwa ni timu inayoongoza kwa kuuza wachezaji kutoka Ureno
Hakuna shaka viongozi wa Yanga wameona kuna kitu kizuri kimefanywa na Benfica ambacho wanadhani wanaweza kukifanya