Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga ambao uliahirishwa jana huenda ukaitishwa Mwezi May 2020 imefahamika
Inaelezwa Mkutano huo umeahirishwa kutokana na matakwa ya Kikatiba ambapo kwa mujibu wa Katiba ya Yanga, uongozi mpya hauna mamlaka ya kuitisha Mkutano Mkuu mpaka watimize Mwaka mmoja madarakani
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla aliitisha Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike Februari 16 kufanya mabadiliko madogo ya Katiba ya Yanga ambapo pamoja na mambo mengine, kubadili mfumo wa uwandikishaji wa Wanachama wa Yanga
Hata hivyo Dk Msolla jana alitoa taarifa ya kusitisha Mkutano huo huku akiwatangazia wanachama wa Yanga kuwa wasubiri taarifa ya tarehe mpya ya kufanyika Mkutano huo
Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kufanyika kwa Mkutano huo kwani wanaamini utakuwa mwanzo wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji wa klabu hiyo