Pengine waamuzi wa Tanzania wanahitaji usaidizi wa VAR ili kuacha kuzibeba timu nyingine huku wakizionea nyingine
Matukio ya uonevu yanayofanywa na waamuzi sasa yanakithiri na kama TFF haitachukua hatua haraka, wanawaweka hatarini hawa waamuzi
Hebu fikiria timu imetoka Lindi, imekuja jijini Dar es salaam inapambana muda mwingi wa mchezo, halafu mwishoni mwamuzi anawanyima haki ya kile walichokipigania kwa utashi wake tu
Itafika siku uvumilivu wa haya matukio utafika kikomo, ni vyema TFF ikajihadhari mapema
Kama nchi imekosa waamuzi wenye kuweza kutafsiri vyema sheria 17 za mpira wa miguu, basi ni vyema ukaangaliwa utaratibu mwingine ambao uaweza kutibu changamoto hii
Lakini pia jambo la kushangaza ni kwa nini ni timu moja tu ambayo inaonekana kunufaika zaidi na makosa ya waamuzi?