Yanga yapinga faini za Bodi ya Ligi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2020
Yanga yapinga faini za Bodi ya Ligi

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko Bodi ya ligi (TPLB) juu ya faini walizopewa katika mechi zao zilizochezwa mwezi uliopita kutokana na kutoridhishwa na jinsi hatua hizo zilivyo chukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari amepam leo, Afisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli ametoa ufafanuzi wa baadhi ya faini ambazo Yanga haikubaliani nazo

Kuhusu kupigwa faini ya shilingi laki tano kutokana na kutowasilisha majina ya wachezaji katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Bumbuli amebainisha kuwa walipeleka kwa kuchelewa kwakuwa mechi ilihamishwa ghafla kutoka uwanja Sokoine kwenda Samora, Iringa baada ya kutokuwa tayari kuchezewa baada ya mvua kunyesha.

Kuhusu faini ya shilingi laki mbili kwa kutoingia kwenye vyumba rasmi katika mchezo dhidi ya Simba msemaji huyo alisema walipeleka malalamiko Bodi ya ligi kuwa vyumba vyao havikuwa salama na wakaruhusiwa kuingia katika vyumba vya timu B, wameshangaa kuona wamepigwa faini hiyo.

Aidha, kuhusu mashabiki wao kurusha chupa za maji katika mchezo huo ni kutokana na wao kupeleka malalamiko Bodi ya juu ya mambo mbalimbali ambayo wanaona wanaonewa lakini hayafanyiwi kazi

Bumbuli ameongeza kuwa wanashangaa Bodi hiyo kuzuia pesa kutoka kwa mdhamini Vodacom bila kufanya majadiliano na klabu hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni ambazo wameziweka wenyewe

Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga umemuita mlinda mlango wao Ramadhani Kabwili baada ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kuwa walitaka kumpa rushwa apate kadi ya njano ili asicheze mchezo unaofuata dhidi ya timu hiyo

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema suala lake ni la jinai hivyo wamemuita ili wakusanye ushahidi ambao wataupeleka kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua za kisheria.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’