Nyota Yanga wamkubali Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2020
Nyota Yanga wamkubali Morrison

Wachezaji wa Yanga wamesifu kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji wao mpya, Bernard Morrison kuwa uwepo wake ni chachu ya mafanikio.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji hao walisema tangu Morrison amejiunga na klabu hiyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kupata matokeo.

Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi alisema ni mchezaji anayejitambua na anajua namna ya kukaa eneo sahihi kwa wakati sahihi na kuweka wazi kuwa ujio wake umeongeza changamoto hasa kwa wachezaji wanaocheza nafasi yake.

"Anaisaidia na ataendelea kuisaidia Yanga kama atabaki na kiwango chake ambacho kimeweza kuwa imara akiwa bado hajazoeana na wachezaji aliowakuta ni nadra sana kwa mchezaji kujiunga na timu na kuzoea mfumo kwa siku chache alizokaa kambini," alisema Tshishimbi.

"Ni mapema sana kuendelea kumsifu, lakini kikubwa watu wanatakiwa kutambua kuwa huyu ni mchezaji mwenye kipaji na si mchezaji wa kutumia nguvu nyingi kufanya mazoezi hivyo waendelee kumuamini na wategemee mambo mazuri zaidi kwa namna mimi nilivyomfuatilia," alisema nahodha huyo.

Naye Mapinduzi Balama alisema anashangazwa na juhudi zake mazoezini kabla ya kufika uwanjani kucheza mchezo wa ushindani kusaka pointi tatu muhimu huku akifichua siri nyingine kuwa wao wanamfaidi zaidi huko na sio uwanjani.

"Siku ya kwanza kufanya mazoezi pamoja sio mimi tu nadhani ni wachezaji wote walikoshwa na kiwango chake Morrison anajua kuchezea mpira anapiga pasi za uhakika ni mchezaji mzuri tunatarajia makubwa kutoka kwake."

Mapinduzi aliongeza kuwa kwa muda mchache waliokaa naye wamebaini kuwa sio mchezaji wa kufundishwa mbinu yeye anajua namna ya kucheza na akili ya kila mchezaji ni muda gani anatakiwa kukaa na mpira mguuni na muda gani atoe pasi kwa mchezaji mwenzake.

MWANASPOTI

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’