Tuko pamoja na Kabwili - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2020
Tuko pamoja na Kabwili - Bumbuli

Uongozi wa Yanga umesema uko pamoja na mlinda lango wake Ramadhani Kabwili ambaye jana alifichua tukio la jaribio la hongo alilofanyiwa na baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba msimu uliopita

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema pamoja na kuwa wachezaji hawaruhusiwi kungea na vyombo vya habari, lakini kwa kuwa Kabwili tayari amelizungumza hili, watampa ushirikiano wote ili kukomesha matukio haya ya rushwa ambayo yanachafua taswira ya soka la Tanzania

Aidha Bumbuli amesema tukio hili lifungue njia kwa wadau wenye ushahidi wa matukio mengine ya rushwa katika soka hapa nchini wajitokeze hadharani ili kukomesha matukio haya

"Sisi kama Yanga tutakaa na Kabwili kuzungumza nae kwa undani, Kabwili ni Mchezaji wa Yanga hivyo tutampa ushirikiano wa kutosha katika hili baada ya kumsikiliza," amesema

"Ni kweli wachezaji hawaruhusiwi kuongea na vyombo vya habari lakini kwa kuwa imetokea na Kabwili ni mchezaji wetu hayo mambo ni ya ndani ya klabu, lakini kuhusu hizo tuhuma tutashirikiana nae kuona mambo kama haya yanakoma kama ni kweli yapo"

"Niwaombe wadau wenye ushahidi pia wajitokeze sio katika hili tu, hata vitendo vingine kama hivi ili tukomeshe mambo kama haya kwenye mpira wetu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
59m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’