Mkurugenzi wa Singida United Festus Sanga amesema kiungo Raphael Daudi ambaye Yanga ilimtoa kwa mkopo kwenda klabu hiyo, bado hajajiunga nao
Festus amesema mpaka sasa hawafahamu alipo nyota huyo licha ya kukamilisha taratibu zote na uongozi wa Yanga
Akizungumzia sintofahamu hiyo, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Yanga ilimtoa Lothi kwa mkopo pamoja na wachezaji wengine
Lakini tofauti na beki Ali Ali, Lothi hakuwasilisha malalamiko yoyote kwa uongozi kama hakubaliani na mpango huo wa kutolewa kwa mkopo au la
Katika hatua nyingine, Bumbuli amewataka wachezaji ambao hawakubali kutolewa kwa mkopo wafike makao makuu ya klabu hiyo kuonana na uongozi na sio kulalamika kupitia vyombo vya habari
"Hatukufurahishwa na alichofanya Ali Ali, alipaswa kufika makao makuu ya klabu kuwasilisha malalamiko yake, suala lake lingepatiwa ufumbuzi haraka. Kulalamika kwenye vyombo vya habari hakutawasaidia, waje ofisini," amesema