Achana na tambo ambazo winga Mrisho Mgasa huwa anazifanya kutokana na uwezo wake wa kusimama juu ya mpira kwa dakika kadhaa
Juzi nyota mpya wa Yanga Barnard Morrison alifanya tukio la aina yake kwenye mchezo dhidi ya Singida United ambapo alisimama juu ya mpira uliokuwa kwenye mwendo
Tukio hilo pamoja na kiwango alichoonyesha kwenye mchezo huo, vimemfanya awe gumzo kila kona kwenye mitandao ya kijamii
Wanayanga wana shauku kubwa kumshuhudia kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Uhuru/Taifa keshokutwa Jumapili
Kwani kama aliweza kuwa bora katika mazingira ya uwanja wa LITI(Namfua), itakuwaje pale shamba la bibi au kule kwa Mkapa?

Ujio wake kwenye kikosi cha Yanga umekuwa na mchango mkubwa kwani pamoja na kazi yake nzuri uwanjani, amerejesha morali ya mashabiki iliyokuwa imepotea baada ya Yanga kufungwa mechi mbili mfululizo