Beki Ali Ali ni miongoni mwa wachezaji waliotolewa kwa mkopo Yanga hata hivyo inaelezwa amegomea mpango huo
Ali ameuomba uongozi wa Yanga umuache awanie nafasi hapohapo Yanga
Kwa sasa Ali ni kama hana nafasi kutokana na kuzidiwa na ushindani wa namba kwenye safu ya ulinzi
Mkongwe Kelvini Yondani, Lamine Moro, Ally Mtoni na Andrew Vicent ndio walinzi wa kati waliobakishwa baada ya Mustafa Suleyman kuachwa huku Ali Ali na Cleofas Sospeter wakitolewa kwa mkopo
Lengo la kuwatoa baadhi ya wachezaji kwa mkopo ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kucheza ili kulinda viwango vyao
Β
ADVERTISE HERE