Mbelgiji anavyoirudisha kwa kasi kampa-kampa tena

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2020
Mbelgiji anavyoirudisha kwa kasi kampa-kampa tena

Wakati Yanga ikinolewa na Hans van Pluijm msimu wa 2014/15 na 2015/16, ilikuwa ikicheza kandanda safi la kuvutia

Ni wakati huo wachezaji kama Thabani Kamusoko walisajiliwa na kuasisi aina ya uchezaji uliopachikwa jina maarufu la kampa-kampatena

Ni soka la pasi fupi fupi ambalo msingi wake ulitawaliwa na viungo mahiri wakati huo Kamusoko, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke kipindi hicho akiwa wa moto kwelikweli akiwa amejiunga Yanga akitokea klabu ya Mbeya City

Lakini baada ya kuondoka Pluijm na kuingia George Lwandamina, chini ya Mzambia huyo Yanga ilibadilika

Lwandamina alitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza pamoja na mipira mirefu

Hata alipokuja Mwinyi Zahera, Yanga haikuwa na mabadiliko ya mbinu za kiuchezaji

Alikuwa Charles Mkwasa aliyeanza kurejesha mfumo wa Pluijm katika muda wake mfupi aliokuwa kocha wa muda Yanga

Lakini ujio wa Luc Eymael, umeanza kubadili kabisa aina ya uchezaji wa Yanga

Katika michezo yake miwili iliyopita, sura na mwelekeo wa Yanga yake imeanza kuonekana

Mbelgiji huyo anapendelea soka la kuvutia, pasi nyingi na kuwapa burudani mashabiki

Katika mazoezi ya kikosi chake, Eymael hapendi wachezaji kukaa na mpira muda mrefu, huangalia muda ambao kila mchezaji anakaa na mpira

Ndio maana Yanga yake imeanza kupiga zile pasi moja moja nyingi

Mchezo dhidi ya Azam Fc, pamoja na kufungwa Yanga ilikuwa bora zaidi, na hata jana ilitawala mchezo dhidi ya Singida United

Ni miaka sasa mashabiki hawakuwa wameishuhudia Yanga ile ya kampa-kampatena, hakuna shaka Eymael anairudisha burudani hiyo Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’