Uongozi wa klabu ya Yanga umesema unasubiri taarifa rasmi kutoka kwa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuhusu adhabu walizopewa na Kamati ya saa 72 jana
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema klabu itatoa tamko lake baada ya kukabidhiwa barua
"Tumeona kupitia runinga taarifa ya kupigwa faini pamoja na wachezaji wetu kufungiwa. Tunasubiri tukabidhiwe barua na TFF ili tuweze kutoa tamko rasmi la klabu," amesema
Jana Yanga ilikumbana na adhabu mbalimbali zikiwemo faini za fedha na wachezaji wake kufungiwa kutokana na makosa yaliyojitokeza katika michezo yake iliyopita
Yanga imepigwa faini ya Tsh 1.2M pamoja na wachezaji wake watatu Mrisho Ngasa, Cleofas Sospeter na Ramadhani Kabwili kufungiwa huku kocha wake mkuu Luc Eymael akipewa onyo