Juzi muda mchache kabla ya Yanga kushuka dimbani kuchuana na Stand United, kocha Mkuu wa timu hiyo George Lwandamina alipata taarifa ya msiba kutoka nchini kwao Zambia.
Lwandamina alifiwa na mtoto wa dada yake lakini hakutaka kutoa taarifa hiyo mpaka pale mchezo huo ulipomalizika.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Lwandamina amesema hatahudhuria msiba huo kutokana na maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo dhidi ya Simba.
Katika mahojianao na MCL Lwandamina amesema anakusudia kuiongoza timu yake kwenye michezo dhidi ya Simba na baadae Singida United halafu ndio aende Zambia kuhani msiba.
"Nilipata taarifa za msiba huo dakika chache kabla ya kuingia uwanjani lakini sikutaka kumwambia mtu,unajua kule nyumbani mimi ni kama kichwa cha familia sasa kwa msiba wa aina yoyote natakiwa kushiriki kwa kiasi kikubwa,"alisema Lwandamina.
"Sitaweza kuondoka kwa namna yoyote na nimeshawaambia viongozi watulie nitawasiliana na ndugu zangu nafikiri watanielewa nataka kuhakikisha timu yangu inangia kwa nguvu Oktoba 28 ili tuweze kupata pointi tatu muhimu."
Yanga inaingia kwenye mchezo dhidi ya Simba Oktoba 28 ikiwa na kiwango kizuri baada ya kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita.
Timu zote zikiwa na alama sawa, mshindi anatarajiwa kuongoza ligi.
Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni amesema msimu huu atahakikisha timu yake inatwaa ubingwa kwa tofauti ya alama na sio mabao kama msimu uliopita

ADVERTISE HERE