Yanga yamkana Kotei, hapati namba kwa Makame

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jan 2020
Yanga yamkana Kotei, hapati namba kwa Makame

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema timu hiyo haikuwa na mpango wa kumsajili kiungo wa zamani wa Simba James Kotei kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari

Nugaz amesema kwa sasa Yanga haihitaji mchezaji aina yake kwani inao wachezaji wazuri

"Taarifa za sisi kutaka kumsajili Kotei hazina ukweli wowote kwani hana kiwango cha kucheza Yanga," Nugaz aliiambia Wasafi Fm

"Tunaye Abdulaziz Makame ambaye yuko katika kiwango kizuri. Kotei hawezi kupata namba kwenye timu yetu"

Nugaz ni kama amejibu kauli aliyotoa Kotei jana kuwa aligoma kujiunga na Yanga kwa kuwa hapendi kuwaudhi mashabiki wa Simba, timu aliyoitumikia kwa misimu mitatu

Inaelezwa Kaizer Chiefs ilikuwa tayari kumtoa kwa mkopo Yanga nyota huyo raia wa Ghana

Kotei amekosa nafasi kwenye kikosi cha Kaizer Chiefs, hajacheza mchezo wowote tangu aliposajiliwa mwezi Julai 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
32m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
40m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’