Yanga ndani mtiti nje mtiti

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jan 2020
Yanga ndani mtiti nje mtiti

Suala la matokeo ni jambo jingine, lakini kwa namna mabosi wa Yanga walivyokiboresha kikosi chao kupitia dirisha dogo litakalofungwa wiki ijayo, imewafanya mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania kuwa moto nje na ndani na wapinzani wao waanze tu kujipanga.

Ujio wa nyota kadhaa ndani ya kikosi cha Yanga, umekifanya kiwe kipana kinachowapa nafasi makocha wao kuamua watumie wachezaji gani, kwani wanaoanza na wale wanaobaki benchi wote wanaonekana kuwa moto uleule unaounguza.

Tayari Yanga imeshasajili wachezaji watano wapya Tariq Seif, Adeyum Saleh, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi na Yikpe Gnamien, huku wakiwa mbioni kumalizana na nyota wengine wawili akiwamo Mkongo, Owe Banyanga Ituku anayesubiri kuanguka saini tu.

Usajili huo umeifanya Yanga iwe na jumla ya wachezaji 33, wanaoweza kutengeneza vikosi vitatu ambavyo kati ya hivyo vyote imara na vinaweza kufunga katika mchezo wowote ule ambao watakutana nao.

Kwa aina ya wachezaji walionao, Yanga inaweza kuanza na kikosi cha kwanza cha wachezaji hawa: Farouk Shikhalo, Paul Godfrey, Adeyum Saleh, Lamine Moro, Kelvin Yondani, Abdulaziz Makame, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Tariq Seif na Patrick Sibomana

Lakini pia inaweza kupanga mziki wake ukiwajumuisha Metacha Mnata, Juma Abdul, Ally Mtoni ‘Sonso’, Moustapha Seleman, Ali Ali, Papy Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Feisal Salum, David Molinga, Yikpe Gnamien na Mapinduzi Balama ‘Kipenseli’.

Achana na vikosi hivyo unaambiwa bado Yanga ina majembe mengine matata baadhi walikipiga juzi kwenye mechi ya Kombe la Mapinduzi na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba.

Kikosi cha tatu cha Yanga kinatengenezwa na kipa Ramadhani Kabwili, Jafary Mohammed, Mharami Issa ‘Marcelo’, Cleofas Sospeter, Andrew Vincent, Said Juma, Juma Mahadhi, Raphael Daud, Said Mussa, Owe Banyanga na Gustapha Saimon.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’