Pamoja na timu yake kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na vijana wake
Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa jana kwenye uwanja wa Taifa, Mkwasa alisema walikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi kwenye kipindi cha pili
"Ulikuwa ni mchezo wa vipindi viwili. Wenzetu wamekaa pamoja kwa muda mrefu na walicheza kitimu zaidi kwenye kipindi cha kwanza, nikiri benchi la ufundi tulikuwa na wakati mgumu sana hasa baada ya kuruhusu bao la pili lakini ari na kujituma kwa wachezaji kulituwezesha kusawazisha mabao yote, nakuhakikishia kama tungepata dakika nyingine chache tungeweza kuibua na ushindi," alisema
"Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani kutoka kwa kila timu, nadhani ni mmoja wa michezo bora ya watani wa jadi"
Mkwasa amesema pamoja na baadhi ya wachezaji hawakuwa na muda mrefu na timu, lakini walifanya vizuri na wamempa matumaini kuwa baada ya muda watakuwa na timu imara sana