Kiungo wa Simba, James Kotei amesema kama watafanikiwa kumdhibiti Papy Kabamba Tshishimbi, mambo yatakuwa magumu kwa Yanga.
Kotei ambaye amecheza michezo karibu yote ya Simba msimu huu, alikiri kuwa katika mechi ya Ngao ya Jamii, Tshishimbi ndiye aliyetibua mipango yao ya ushindi lakini amedai kuwa alikuwa bado hajakumbana na ugumu wa Ligi Kuu hivyo katika mechi ya Oktoba 28 hatakuwa moto tena.
Kiungo huyo raia wa Ghana alifichua kuwa Yanga ya sasa inamtegemea sana Tshishimbi tofauti na msimu uliopita ambapo Haruna Niyonzima na Saimon Msuva ndiyo walikuwa tishio zaidi.
"Aling'ara katika mechi iliyopita kwa kuwa alikuwa ndiyo kwanza ameingia nchini, hakuwa amekutana na ugumu wa Ligi, pia tulimwacha sana acheze peke yake na ndiyo sababu alituvuruga," Kotei amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti.
Kwa maoni yake anaona Yanga inamtegemea mchezaji mmoja, lakini sivyo kwa sasa Yanga imekuwa ikicheza kitimu zaidi kuliko ilivyoanza ligi.

ADVERTISE HERE