FT : Simba 2-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2020
FT : Simba 2-2 Yanga

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga wamefanya 'come-back' ya kibabe baada ya kutokea nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba

Ulikuwa ni mchezo ambao kikosi cha Yanga kilionyesha ukomavu wa hali ya juu

Mchezo huo ulianza taratibu huku kila timu ikicheza kwa tahadhari kubwa

Simba ilifunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 43 kupitia mkwaju wa penati ambao ulikuwa na utata

Mshambuliaji Meddie Kagere alionekana kufanyiwa madhambi nje ya eneo la 18 lakini alimrubuni mwamuzi kwa kujirusha ndani ya box na mwamuzi Jonesia Rukyaa kutoa mkwaju wa penati

Dakika moja baada ya kipindi cha pili Simba ilifunga bao la pili kupitia kwa Deo Kanda

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Yanga ambayo ilitandaza kandanda safi ya kuweza kujipatia bao la kwanza kwenye dakika ya 50 kupitia kwa Mapinduzi Balama

Dakika tatu baadae, Mohammed Issa 'Banka' akaisawazishia Yanga kwa kufunga bao la pili kwenye dakika ya 54

Uamuzi wa Jonesia kuwapa peneti Simba uliwakera mashabiki ambao walimtupia chupa za maji baada ya mchezo huo kumalizika

Pamoja na mchezo huo kumalizika kwa sare, Yanga ilikuwa bora na hakika wamezima tambo za wapinzani wao Simba waliokuwa wakitamba kuwa wangeondoka na ushindi mnono leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’