Yanga itashuka dimbani Jumapili, Oktoba 22 ugenini kucheza na Stand United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa saba.
Baada ya Simba na Mtibwa Sugar kupata ushindi katika michezo yao ya mzunguuko wa saba, timu hizo zimefikisha alama 15.
Yanga nayo inaweza kufikisha idadi hiyo kama itapata ushindi dhidi ya Stand United.
Japo bado changamoto katika upachikaji wa mabao inahitaji kupatiwa ufumbuzi, kwa sasa ni muhimu timu kupata ushindi kwanza ili kwenda sambamba na vinara wa ligi.
Msimu huu ni moja ya misimu ambayo Yanga imefunga mabao machache katika hatua hii pengine kuliko wakati mwingine wowote.
Kwa sasa ni vyema timu ishinde kwa idadi yoyote ya mabao wakati benchi la ufundi likiendelea kuboresha safu ya ushambuliaji.
Haitakuwa jambo la kushangaza mwezi ujao wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Yanga ikashusha washambuliaji wengine kuchukua nafasi za wale ambao wameshindwa kuisaidia timu kutokana na majeruhi ya mara ya kwa mara
Bila shaka katika mchezo wa Jumapili, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib wataendelea kuibeba safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Wawili hao walionyesha ushirikiano mzuri katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na bila shaka watafanya kweli katika mchezo huo wa Jumapili.

ADVERTISE HERE