Niyonzima aomba sapoti ya mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jan 2020
Niyonzima aomba sapoti ya mashabiki Yanga

Kiungo Haruna Niyonzima amesema anajisikia faraja kurejea nchini kujiunga tena na Yanga, timu aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia Simba mwaka 2017

Niyonzima anatarajiwa kuwasili nchini leo kuungana na mabingwa hao wa kihistoria huku kukiwa na taarifa kuwa anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Simba Jumamosi

Niyonzima amewataka mashabiki kusahau yaliyopita, wafungue ukurasa mpya wa ushirikiano ili kuhakikisha wanafikia malengo ya timu

"Nakuja leo Tanzania kuungana na timu yangu (Yanga), kurejea nyumbani hiyo ni ishara kuwa nipo tayari kuwafanyia kazi kwa hiyo kama kuna makosa yalitokea awali naomba tuyasahau," amesema Niyonzima

"Naomba ushirikiano na upendo kama niliopewa kipindi nakuja kujiunga Yanga kwa mara ya kwanza"

"Nipo tayari hata kwa mchezo dhidi ya Simba japo sipendi kuongelea sana kwa maana mechi hizi zina mambo mengi sana lakini kikubwa ni kujiandaa kisaikolojia"

Niyonzima aliitumia Yanga kwa miaka sita tangu mwaka 2011 kabla ya kutimkia klabu ya Simba mwaka 2017

Anarejea Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wa miezi sita na klabu ya AS Kigali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’