Niyonzima tutampokea Jumatano - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Dec 2019
Niyonzima tutampokea Jumatano - Nugaz

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kiungo Haruna Niyonzima atawasili kesho Jumatano kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria

Nugaz amesema wataandaa utaratibu maalum wa kumpokea kiungo huyo fundi ambaye ujio wake ulianza kutangazwa tangu juzi

"Niyonzima atawasili siku ya Jumatano, panapo majaaliwa tunaweza kumtumia kwenye mchezo dhidi ya watani zetu Simba siku ya Jumamosi," amesema Nugaz

"Tutaandaa utaratibu maalum kwa mashabiki kumpokea na kumkaribisha Yanga kwa mara ya pili"

Usajili wa kutikisa nchi unakuja

Katika hatua nyingine, Nugaz amesema bado GSM hawajafunga usajili kwani wanatarajia kumshusha nyota ambaye usajili wake utatikisa nchi

"Bado kuna 'big signing' moja inakuja. Tunashusha jembe ambalo litawalaza watu na viatu mapemaaa," alitamba Nugaz

Milioni 50 kutolewa mchezo dhidi ya Simba

Ukiwa ni utaratibu wa uhamasishaji ambao wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM wamejiwekea, mchezo dhidi ya Simba wataweka mezani kitita cha Tsh Milioni 50 badala ya Milioni 10 ambazo wameweka michezo iliyopita

"GSM wameweka kwenye ubao Tsh Milioni 50 ili kuhakikisha mnyama anakufa Jumamosi, fedha hizo nitazikabidhi mwenyewee..," aisema Nugaz

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’