Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga huwa na msisimko mkubwa sana
Ni katika mchezo huu hushuhudiwa matukio yasiyo ya kawaida
Ukweli ni kwamba kipimo halisi cha mapenzi ya mashabiki kwa timu zao utakipata hapa
Sasa mashabiki watatu wa Yanga kutoka mkoani Mtwara, wameianza safari kuelekea jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo aina ya timu hizo ambao utapigwa Januari 04 2020
Mashabiki hao wanakwenda jijini Dar es salaam kwa kutumia usafiri wa baiskeli
Uongozi wa Yanga umewaandalia mapokezi makubwa mashabiki hao ikiwa ni pamoja na kuwakatia tiketi na kuwapatia jezi origino za Yanga brand chapa GSM
Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema tukio hilo ni la kihistoria, hivyo nao watawaenzi mashabiki hao kwa kutambua thamani waliyoipa Yanga
"Yanga Makao Makuu itawapokea kwa furaha na Amani na vile vile tutawapatia tiketi za kuuona mchezo wetu dhidi ya Watani wetu,Jezi mpyaa Brand Chapa GSM kwa wote watatu na kifuta jasho tulichokiandaa kwa ajili yao"