Mustafa Suleyman bado yupo sana Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2019
Mustafa Suleyman bado yupo sana Yanga

Katika michezo miwili iliyopita Kaimu kocha mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amemtumia beki Mustafa Suleyman safu ya ulinzi wa kulia

Ni baada ya kumkosa Juma Abdul ambaye alichelewa kujiunga na timu kutokana na ushiriki wake wa michuano ya Chalenji na timu ya Taifa ya Tanzania Bara

Lakini pia Paulo Godfrey Boxer aliyekuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi mitatu, bado hayuko fiti hivyo Mkwasa analazimika kumtumia kwa tahadhari

Mustafa ambaye tetesi zilishamiri kuwa alikuwa kwenye mpango wa kuachwa dirisha dogo, ni kama amepindua meza kibabe, kwani anaonekana kuimarisha kiwango chake

Katika michezo miwili aliyocheza, ameonekana kutimiza vyema majukumu ya ulinzi

Ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kukaba, ni aina ya mabeki ambao wanaweza kupewa kazi maalum ya kukaba washambuliaji wasumbufu

Huyu anaiweza kazi aliyokuwa akipewa beki Abdallah Shaibu 'Ninja' kwenye mechi za Yanga na Simba wakati wa kocha Zahera msimu uliopita

Bila shaka, Mustafa ataendelea kubaki katika viunga vya Yanga kwa muda mrefu kuliko ilivyokuwa ikidhaniwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’