Pamoja na kushindwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya CIity, kiungo mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana 'PS' amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akiwahakikishia kuwa matokeo mazuri yanakuja
Aidha Sibomana amesifu upambanaji uliionyeshwa na wachezaji wenzake kwenye mchezo huo uliopigwa katika mazingira magumu ya uwanja wa Sokoine
"Ingawa hatukuweza kushinda lakini mnapaswa kutuamini kwani tuna uhakika matokeo mazuri yanakuja," amesema
Ni mchezo ambao kila shabiki alikuwa na shauku ya kuona mabingwa hao wa kihistoria wanaondoka na alama zote tatu
Lakini kwa kiasi kikubwa wachezaji walionyesha ari ya kupambana, ni bahati mbaya ushindi haukupatikana
Spiriti hiyo inapaswa kuendelezwa zaidi kwenye mchezo wa Ijumaa dhidi ya Prisons