Kuelekea mpambano wa watani wa jadi wiki ijayo, homa imeanza kupanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2017
Kuelekea mpambano wa watani wa jadi wiki ijayo, homa imeanza kupanda
Tanzania inaweza kusimama kwa muda Jumamosi, Oktoba 28 kupisha pambano la watani wa jadi Simba na Yanga ambalo limepangwa kupigwa uwanja wa Uhuru kuanzia saa 10: 00 za jioni.

Yanga ndio watakuwa wenyeji wa mpambano huo ambao umeteka hisia za wadau wengi wa soka nchini lakini wataingia uwanjani wakiwa tayari na nguvu ya kujiamini kutokana kupata matokeo mazuri kwenye michezo ya hivi karibuni.

Ukali wa pambano hilo hauna tofauti na ule wa La Liga kule nchini Hispania kati ya Real Madrid na FC Barcelona au pale England baina ya Manchester United na Manchester City na kule Italia unaweza kusema ni AC Milan na Inter Milan.

Ukilinganisha na miaka ya nyuma clasico ya msimu huu inatarajiwa kuongeza ushindani kutokana na matokeo ya msimu uliopita ambapo Simba iliweza 'kuinyanyasa' Yanga katika michezo yote ya mashindano baina ya timu hizo.

Msimu uliopita Yanga iliambulia sare kwenye mchezo mmoja na kisha kupoteza mchezo mmoja kwenye ligi, kupoteza mchezo kwenye kombe la Mapinduzi na mwanzoni mwa msimu huu kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii.

Ni dhahiri kocha wa Yanga George Lwandamina hakuna matokeo atahitaji kwenye mchezo huo zaidi ya ushindi ili kwanza afute uteja mbele ya mwenzake Omog pili aongeze usalama wa kibarua chake.

Michezo ya Simba na Yanga inaongoza kwa kuwafukuzisha makocha na kwa hali ilivyo timu itakayofungwa siku hiyo kocha wake atakuwa amejikatia tiketi mapema.

Sasa wakati zikiwa zimesalia takribani siku tisa kuelekea mchezo huo tayari makocha George Lwandamina wa Yanga na Joseph Omog wa Simba wameanza kuipigia mahesabu mechi hiyo.

Kabla ya timu hizo kukutana, zinakabiliwa na mechi za ligi wikiendi hii ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa Njombe Mji keshokutwa Jumamosi wakati Yanga itakuwa ugenini kuikabili Stand United Jumapili.

Haitakuwa jambo la kushangaza kwa walimu kufanya marekebisho ya vikosi vyao vinavyocheza wikiendi hii ili kuhakikisha wanaingia kwenye mpambano huo wakiwa na vikosi imara.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’