Kelvin Yondani na Juma Abdul wako hatarini kuukosa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba kama watapata kadi za njano kwenye mchezo dhidi ya Stand United Oktoba 22.
Walinzi hao wa kutumainiwa wote wana kadi mbili za njano ambapo wote walipata kadi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Ili kuhakikisha wachezaji hao hawaukosi mchezo dhidi ya Simba huenda kocha George Lwandamina akalazimika kuwapumzisha kwenye mchezo dhidi ya Stand United.
Jana Yanga ilicheza na Rhino Rangers mchezo wa kirafiki ambapo nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' alicheza nafasi ya Yondani wakati Hassani Kessy alicheza badala ya Juma Abdul.
Wawili hao huenda wakatumika katika mchezo ujao dhidi ya Stand United.

ADVERTISE HERE