Yanga yakomaa kumbakisha Lamine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Dec 2019
Yanga yakomaa kumbakisha Lamine

Uongozi wa klabu Yanga umesema hauna mpango wa kumuacha beki wao kisiki Lamine Moro ambaye aliandika barua ya kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya mishahara

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amekiri beki huyo kuwa na madai ya mishahara miwili na sio mitatu

"Lamine bado ni mchezaji wetu kwani ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Madai yake ya mishahara ya miezi miwili pamoja na wachezaji wengine wote watalipwa leo," amesema

Ataja sababu ya kumtema Sadney

Aidha Dk Msolla amesema uongozi umeamua kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake Sadney Urikhob kutokana na uwezo wake kutoendana na matarajio ya klabu

Dk Msolla amesema Sadney aliomba mkataba wake kuvunjwa na uongozi uliridhia kwa kuwa hakuweza kufikia matarajio ya timu

"Tumemwachia Sadney kwakuwa uwezo wake ni mdogo lakini tunapambana kumzuia Lamine Moro asiondoke. Mpira ni mchezo wa wazi , uwezo wa beki huyu kila mtu ameuona"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’