Msimu uliopita kikosi cha timu ya Wanawake Yanga Princess haikuwa bora, ikimaliza miongoni mwa nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi
Lakini kufuatia maboresho yaliyofanyika, kikosi cha Yanga Princess kiko imara pengine ni moja ya timu ambazo msimu huu zitawania kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Wanawaka maarufu kama Serengeti Lite
Msimu huu Yanga Princess imeshinda mechi zote tatu, wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama tisa
Wametofautiana mabao na Alliance Girls ambao wana tofauti ya mabao 10 wakati Yanga Princess wakiwa na tofauti ya mabao 7

Mchezo unaofuata ni dhidi ya Simba Queens na utapigwa Disemba 14 kwenye uwanja wa Uhuru
ADVERTISE HERE