Yanga kamili kuikabili KMC leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2019
Yanga kamili kuikabili KMC leo

Kikosi cha Yanga leo Jumatatu, Disemba 02 2019, saa kumi jioni kitashuka katika uwanja wa Taifa kuchuana na KMC ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Baada ya kushinda mechi tano mfululizo, mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wakisaka ushindi mwingine muhimu ambao pia utakuwa ushindi wa nne mfululizo kwa kocha Charles Boniface Mkwasa 'Master'

Akizungumzia maandalizi ya timu yake, Mkwasa amesema wamejipanga kuendeleza wimbi la ushindi leo

Hata hivyo amekiri mchezo hautakuwa mwepesi kwani pamoja na kuwa na KMC wana mwenendo wa kusuasua, sio wabaya

"KMC ni moja kati ya timu bora kwenye ligi yetu tangu ipande ligi Kuu"

"Pamoja haijafanya vyema kwenye mechi zake za hivi karibuni, tunatambua sana kuwa mchezo utakuwa mgumu na wa ushindani ila vijana wapo tayari kuwakabili wapinzani wetu na kuondoka na alama zote tatu," amesema Mkwasa

Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu yao

Ametaja viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-

Aidha Nugaz amesema kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, wameweka mezani Tsh Milioni 10 kwa ajili ya wachezaji kama wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo

Umekuwa ni utaratibu GSM kutoa kiasi hicho cha fedha kwa kila mchezo wa ligi ambao Yanga inashinda

Tayari wametoa Tsh Milioni 50 ushindi mechi dhidi ya Coastal Union, Mbao Fc, Ndanda Fc, JKT Tanzania na Alliance FC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’