Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuikabili KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2019
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuikabili KMC

Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Taifa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC

Mchezo huo ambao utapigwa kesho Jumatatu Disemba 02, umehamishiwa uwanja wa Taifa kutoka uwanja wa Uhuru ambao ulitarajiwa kupigwa awali

Kaimu kocha mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wamefanya maandalizi mazuri, wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo

Huo utakuwa mchezo wa nne Mkwasa anakiongoza kikosi cha Yanga tangu akabidhiwe timu mapema mwezi huu

Ameshinda mechi zote tatu zilizopita dhidi ya Ndanda Fc, JKT Tanzania na Alliance Fc

Katika mchezo huo Yanga itawakosa nyota wake wanne Abdulaziz Makame, Feisal Salum, Mohammed Issa 'Banka' na Ally Ally ambao wako na timu ya Taifa ya Zanzibar

Paulo Godfrey na Juma Mahadhi nao wanatarajiwa kukosekana

Matokeo ya ushindi kesho yataipandisha Yanga hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’