Vyombo vya habari Zambia vyaripoti kuachwa kwa Kalengo Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2019
Vyombo vya habari Zambia vyaripoti kuachwa kwa Kalengo Yanga

Mtandao wa Zambianfootball umeripoti kuachwa kwa mshambuliaji Maybin Kalengo aliyekuwa akiitumikia Yanga akitokea klabu ya Zesco United

Kalengo aliyepata majeraha ya kuvunjika mguu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc mwezi Oktoba, ameitumikia Yanga kwa miezi sita tu

"Kalengo mwenye umri wa miaka 21 alishindwa kuonyesha makali kwa Wana Jangwani hao tangu alipojiunga nao mwishoni mwa mwezi wa sita. Amerejea nyumbani karibuni kuuguza majeraha. Taarifa zimebainisha kuwa ameambiwa asirejee katika klabu hiyo," wameripoti zambianfootball

Yanga imejipanga kuimarisha kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo linalofunguliwa Disemba 16

Wataitumia nafasi ya Kalengo kusajili mshambuliaji mwingine

Aidha Issa Bigirimana 'Walcott' ni nyota mwingine ambaye anaweza kuachwa

Mapema mwezi huu Bigirimana alipewa ruhusa ya kurejea kwao kama ilivyo kwa Kalengo kushughulikia matatizo binafasi

Licha ya kurejea nchini, Uongozi wa Yanga umemtaka ajieleze baada ya kuchelewa kurudi

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alimzuia kufanya mazoezi hadi hapo atakapomalizana na uongozi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’