Mwakalebela amuita Zahera Makao Makuu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Nov 2019
Mwakalebela amuita Zahera Makao Makuu Yanga

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amemkaribisha Makao Makuu ya klabu hiyo Mwinyi Zahera aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo

Zahera amerejea nchini leo kwa kile alichoeleza kuja kufuatilia madai yake katika klabu ya Yanga

Mwakalebela amesema hawana tatizo na Zahera na wanamkaribisha Jangwani kwa ajili ya majadiliano ya suala lake

"Tumesikia yuko nchini kupitia vyombo vya habari, tunamkaribisha afike ofisini kwetu kwani ndio sehemu sahihi ambayo hilo lililomleta linaweza kuzungumzwa," amesema

"Tunafahamu alikuwa kocha wetu, sisi kama Yanga hatuna tatizo nae, afike tu ofisini"

Baada ya kutua nchini Zahera amedai kuja kuchukua fedha zake Yanga pamoja na kusaini barua ya kuvunja mkataba ambayo hakuisaini awali

Tangu kuvunjwa mkataba wake Zahera amekuwa akiushushia tuhuma mbalimbali uongozi wa Yanga jambo ambalo limeonekana kuwakera viongozi hao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’