Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wataongeza umakini katika michakato yao ya usajili ili kuhakikisha wachezaji wanaosajili wanakuwa na viwango vya kucheza timu hiyo
Mkwasa amesema Yanga ina mifumo ya kutengeneza wachezaji wake wa ndani lakini kwa wale wanaotoka nje lazima wawe na uwezo
"Tutaweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wachezaji tunaowasajili wana ubora. Hapa sisi kwetu hatuleti mchezaji kwa ajili ya kujifunza au kujiendeleza," amesema
"Tunahitaji wachezaji wenye uwezo ambao wakija hapa wanakuja kufanya kazi moja kwa moja"
"Tunajipanga kwa kushirikiana na Kamati ya Usajili na uongozi wa juu kuandaa utaratibu ambao utasaidia kusajili wachezaji ambao tunadhani watatusaidia katika nafasi ambazo tuna mapungufu"
Msimu huu Yanga imesajili nyota tisa wapya wa kigeni lakini miongoni mwao ni beki Lamine Moro, mlinda lango Farouk Shikhalo na Patrick Sibomana ambao wameonyesha uwezo unaoridhisha
Nyota wengine kama David Molinga, Sadney Urikhob na Juma Balinya wamekuwa wakiimarika taratibu huku kukiwa na uwezekano kwa Mustafa Suleyman, Issa Bigirimana na Maybin Kalengo kupewa mkono wa kwaheri wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa Disemba 16