Tetesi : Bigirimana, Kalengo 'wamesepa mazima'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2019
Tetesi : Bigirimana, Kalengo 'wamesepa mazima'

Taarifa za kuaminikia kutoka ndani ya viunga vya Yanga imebainisha kuwa nyota Issa Bigirimana na Maybin Kalengo hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kuelekea usajili wa dirisha dogo

Nyota hao walipewa ruhusa kurejea makwao wakikabiliwa na changamoto za majeruhi, huenda wasirudi tena

Imebainika kuwa Kalengo alitua Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja

Baada ya kupata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu, Yanga italipia gharama za matibabu yake lakini inamrejesha katika klabu yake ya Zesco United

Inaelezwa Bigirimana hakufikia makubaliano yaliyowekwa katika mkataba wake, Yanga imeona kuendelea kuwa nae ni hasara kwani muda mwingi amekuwa majeruhi

Nyota mwingine ambaye amekalia kuti kavu ni beki Mustafa Suleyman ambaye kiwango chake bado hakiwashawishi mabosi wa Yanga

Walinzi wazawa Ally Ally na Ally Mtoni wameonyesha kuwa na uwezo zaidi yake hivyo haitakuwa rahisi kwake kuendelea kubaki Yanga wakati hana uhakika wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku akiwa mchezaji wa kigeni

Mustafa alipaswa kuwapa changamoto wachezaji wazawa lakini imekuwa tofauti, wachezaji wazawa wanampa changamoto yeye

Ni dhahiri Yanga itakuwa na nafasi sio chini ya tatu, kuongeza nyota wa kigeni dirisha dogo

Tetesi zimekuwa nyingi kuhusu nyota wa kigeni ambao wanatajwa kuwa watasajiliwa

Kila kitu kitakuwa wazi katika kipindi cha wiki tatu pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Disemba 16

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’