Mkwasa amtaka Molinga atulize 'mzuka'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Nov 2019
Mkwasa amtaka Molinga atulize 'mzuka'

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo David Molinga kutulia inapotokea anafanyiwa mabadiliko

Molinga ni mchezaji asiyependa kutolewa uwanjani na mara nyingi anapofanyiwa mabadiliko huonyesha hasira zake waziwazi

Ni tabia ambayo hakuianza wakati huu wa Mkwasa, hata wakati Yanga ikinolewa na Mwinyi Zahera alifanya hivyo

Mkwasa amesema mabadiliko yanayofanyika mara nyingi yanakuwa na lengo la kuiweka timu sawa baada ya kubaini mapungufu ya mchezaji au mbinu za mchezo

"Sio jambo jema kuonyesha utovu wa nidhamu pale mchezaji anapofanyiwa mabadiliko. Benchi la ufundi ndilo linafahamu mahitaji ya mchezo hivyo suala la mabadiliko halifanywi tu kwa utashi wa kocha, kunakuwa na sababu," alisema Mkwasa

"Molinga atulie, tuna mechi nyingi sana.. lakini pia kutolewa haimaanishi kuwa mchezaji amefanya vibaya, wakati mwingine ni mabadiliko ya mbinu tu"

Mkwasa alimtoa Molinga kwenye dakika ya 67 ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulaziz Makame 'Bui'

Mkwasa aliondoa mshambuliaji na kuongeza kiungo katika jitihada za kuimarisha safu ya kiungo ambayo ilikuwa imetawaliwa na JKT Tanzania katika kipindi cha pili

Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga kulinda ushindi wa mabao 3-2 waliokuwa wameupata kwenye kipindi cha kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’