FT : Yanga 3-2 JKT Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2019
FT : Yanga 3-2 JKT Tanzania

Yanga imeendeleza rekodi ya ushindi chini ya kocha Charles Mkwasa baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali, uliilazimu Yanga kufanya kazi ya ziada kulinda ushindi wake kwenye kipindi cha pili

Pamoja na kuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza, makosa ya hapa na pale yaliyofanywa na safu ya ulinzi, yaliiacha Yanga ikienda mapumziko kwa uongozi wa mabao 3-2

Ilitangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Patrick Sibomana 'PS' kabla Adam Adam hajaisawazishia JKT Tanzania dakika chache baadae

Bao la pili la Yanga liliwekwa kimiani na Juma Balinya kisha David Molinga kuongeza bao la tatu kupitia mpira wa adhabu nje kidogo ya 18

Hata hivyo Danny Lyanga alipunguza uongozi wa Yanga na kubaki tofauti ya bao moja kwenye dakika ya 45 akifunga bao rahisi lililotokana na safu ya ulinzi kutokuwa makini

Katika mchezo huo kiungo Mapinduzi Balama alipata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Mohammed Issa 'Banka'

Baadae Abdulaziz Makame na Mrisho Ngasa waliingia kuchukua nafasi za David Molinga na Patrick Sibomana

Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 13 baada ya kushuka dimbani mara sita

Imepata ushindi katika michezo yote minne iliyopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’