Kagera Sugar kesho Jumamosi itashuka katika dimba lake la Kaitaba kuwakabili mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga.
Kagera Sugar bado haijashinda mchezo hata mmoja katika mechi tano ilizocheza za ligi kuu tangu kuanza kwa msimu huu. Bado wapo kwenye harakati za kutafuta ushindi wao wa kwanza msimu huu.
Endapo Kagera Sugar itashinda dhidi ya Yanga, utakuwa ni ushindi wao wa kwanza msimu huu (2017/2018).
Historia inaonesha Kagera hawana rekodi nzuri kwa Yanga, katika mechi tano zilizopita wamefungwa zote huku kipigo kibaya kwao kikiwa ni cha msimu uliopita kwenye uwanja wao walipokubali kulazwa 6-2 kama wamesimama.
Mara ya Mwisho Kagera kupata ushindi dhidi ya Yanga ilikuwa ni 2014 miaka mitatu iliyopita.

ADVERTISE HERE