Tshishimbi afurahi kurudishwa namba sita

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2019
Tshishimbi afurahi kurudishwa namba sita

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema 'ana-enjoy' kucheza namba sita na amefurahi baada ya Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kumrudisha katika nafasi hiyo

Tangu Mkwasa akabidhiwe majukumu ya kuionoa Yanga, moja ya mabadiliko aliyofanya ni kumrudisha Tshishimbi namba sita

Wakati wa kocha Mwinyi Zahera, Tshishimbi alitumika kama mchezaji kiraka wakati mwingine akicheza namba 10

Mwenyewe amesema pamoja na kuwa tayari kucheza nafasi yoyote ambayo atapangwa na kocha, lakini namba sita ndio ya kwake zaidi

"Mimi naweza kucheza popote ambapo kocha ananiambia nicheze, lakini kuna namba yangu ambayo nikicheza na-enjoy," Tshishimbi aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union

"Kocha Mkwasa wakati nakuja Yanga yeye alikuwa Katibu Mkuu, anafahamu na alikuwa anapendelea nikicheza namba sita, nimefurahi kuwa amenirudisha kucheza nafasi hiyo"

"Nikicheza namba sita nakuwa huru, kwa sababu ni nafasi ninayopenda zaidi kucheza"

Tshishimbi alifunga moja ya mabao ya Yanga kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’