Baada ya hapo jana kutimba Kariakoo na kuwanasa wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanaouza jezi feki, zoezi limeendelea leo kwa maafisa wa jeshi la Polisi, GSM na vongozi wa Yanga kutimba katika godauni za wasambazaji wakubwa wa bidhaa za michezo
Afisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamedhamiria kuwanasa wote wanaohusika na biashara hiyo jijini Dar es salaam
"Tunaendelea na kampeni ya kamata-kamata ya jezi feki, leo tumeingia katika godauni za wasambazaji wa vifaa vya michezo," amesema
"Tunapita kila godauni kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama hawana mizigo ya jezi feki"
"Tunawaambia wote wanaohusika na biashara hiyo waache kwani ukaguzi huu unaendelea. Umefika wakati Yanga inastahili kunufaika na bidhaa zake hatutaruhusu wajanja wachache kujinufaisha kupitia mgongo wa Yanga"