Malinzi akumbana na rungu la FIFA, afungiwa miaka 10

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Nov 2019
Malinzi akumbana na rungu la FIFA, afungiwa miaka 10

Wakati akiwa bado anashikiliwa kwa mashitaka mbalimbali yakiwemo ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha, Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi amekumbana na 'rungu' la FIFA baada ya kufungiwa miaka 10

Jana Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) lilitangaza kumfungia kwa miaka kumi (10) Malinzi baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.

Mbali na adhabu hiyo, Malinzi pia amepigwa faini ya Dola za Kimarekani 503,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.1 za Kitanzania.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Maadili ya FIFA baada ya uchunguzi uliobaini kuwa Malinzi alihusika katika matumizi mabaya ya fedha za FIFA (FIFA Financial Assistance Programme (FAP) funds), fedha za CAF, fedha nyingine za TFF pamoja na kughushi nyaraka za maazimio ya Kamati ya Utendaji ya TFF kati ya mwaka 2013 na 2017.

Adhabu hiyo inaanza kufanya kazi kuanzia Novemba 8, 2019 na tayari Malinzi mwenyewe ameshajulishwa.

"Kamati imemkuta na hatia ya kuvunja kanuni ya 24 inayohusu kughushi nyaraka, na kanuni ya 28 inayohusu matumizi mabaya ya fedha katika kanuni za maadili ya FIFA toleo la mwaka 2018 na hivyo inamfungia miaka kumi kujihusisha za shughuli zote za soka Kitaifa na Kimataifa" imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na FIFA.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’