Baada ya kutimuliwa, Zahera aanza kufunguka na ndani Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2019
Baada ya kutimuliwa, Zahera aanza kufunguka na ndani Yanga

Akihojiwa mapema leo eFM radio, aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameushukia uongozi wa timu hiyo kuwa ulishindwa kuihudumia timu

Zahera amesema timu hiyo ilipata changamoto ilipokwenda kucheza mechi za ligi ya mabingwa nchini Botswana na Zambia

Amesema viongozi walishindwa kuhudumia timu Botswana ambapo walilazimika kupanda basi kutoka Afrika Kusini mpaka Gaborone

Lakini pia viongozi walishindwa kulipa baadhi ya gharama za chakula

Pia Zahera amesema kuwa hali kama hiyo ilijitokeza Zambia, alilazimika kutoa pesa zake kwa ajili ya chakula na uwanja wa mazoezi

Aidha, katika mchezo uliofanyika uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Pyramid Fc,Β  viongozi waliipeleka timu katika Hotel isiyo na utulivu hali iliyomfanya yeye mwenyewe awasiliane na viongozi wa GSM kutatua tatizo hilo

Mkoani Mwanza, Zahera amesema alilipa gharamaΒ  ya vinywaji ambayo viongozi wa Yanga walishindwa kuilipa

Hata katika masuala ya usajili Zahera amesema alitumia fedha zake, uongozi ukiahidi kumrudishia

Mcongomani huyo pia ameushushia lawama uongozi wa Yanga kwa kuingilia majukumu ya benchi la ufundi

Amesema moja ya sababu iliyopelekea msimu uliopita wakafanya vizuri, ni viongozi kujitenga na masuala ya benchi la ufundi hali ambayo amesema imekuwa tofauti wakati huu wa uongozi mpya

Amesema hana kinyongo kuondoka Yanga, anajivunia mafanikio aliyoipa timu hiyo msimu uliopita

Hata hivyo kocha huyo anasubiri kulipwa fedha zake za kuvunjiwa mkataba pamoja na madeni ambayo Yanga ilikuwa ikikopa kwake...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’