Baada ya kurejea kutoka Misri hapo jana, kikosi cha Yanga leo kimeendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa Ijumaa, Novemba 08 mkoani Mtwara
Pamoja na tetesi kushika kasi kuhusu hatma yake, kocha Mwinyi Zahera ameendelea na majukumu yake ya kuinoa timu hiyo ambapo amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa watarudi na alama tatu kutoka Mtwara
Yanga inatarajiwa kuelekea Mtwara keshokutwa Alhamisi tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Ijumaa
Mabingwa hao wa kihistoria wanashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama saba baada ya kushuka dimbani mara nne
Hata hivyo wana michezo sita ya viporo
ADVERTISE HERE